BENIEL
SEKA
Tarehe
22 Julai ni siku ya kadirio la pai. Huenda siku hiyo imepita bila wengi wenu
kugundua. Hii inawezekana imetokana na baadhi yenu kutojua kuwepo kwa siku hiyo
au siku hiyo kutokuwa na shamrashamra za kuifanya ijulikane. Hata hivyo makala
hii inakusudia kukufahamisha kuhusu siku hiyo ili wakati ujao uweze kuienzi au
kuisherehekea.
Wengi wenu bila shaka mtakumbuka kwamba
tarehe 14 Machi ni siku ya pai. Hii inatokana na thamani ya pai kwa nafasi mbili
za desimali ambayo ni 3.14. Tatu inatumika kuwakilisha mwezi wa 3 wa mwaka
ambao ni Machi na 14 inawakilisha siku ya 14 ya mwezi huo. Siku hiyo
ilipendekezwa na walimu wa hisabati kwa mara ya kwanza huko San Frasisco
Marikani na kuungwa mkono na wanahisabati katika nchi kadhaa duniani. Tanzania
ilianza kuisherehekea siku hiyo tangu 2004.
Kuanzishwa kwa siku hiyo kuliamsha mjadala
kwa nini 3.14 ipewe siku maalumu wakati kuna kadirio jingine la pai ambalo ni
22 juu ya saba. Hata wanafunzi shuleni huambiwa pai ni 22 juu ya 7 au 3.14. Namba
hizo mbili hutumika wakati wa kukokotoa eneo la umbo duara, mzingo wa duara,
eneo na ukubwa (ujazo) wa mche duara na kadhalika. Kwa mantiki hiyo,
ilikubaliwa kuwe na siku nyingine kwa ajili ya pai ambayo ilipendekezwa iwe 22
Julai na iitwe SIKU YA KADIRIO LA PAI.
Kwa wale ambao mmekuwa mnafuatilia sherehe
za pai mtakumbuka kwamba Tanzania imekwisha sherehekea siku ya pai kwa mara tisa
na. kiasi miaka inavyokwenda ndio msisimko wa pai unavyoongezeka na sherehe
kuzidi kufana. Wale mlioshnudia sherehe ya mwaka huu mnakumbuka jinsi walimu,
wanafunzi , wahadhiri wa vyuo vikuu, wakufunzi wa vyuo vya ualimu na wadau
mbalimbali walivyofanya matembezi ya hiari kutoka shule ya sekondari ya
Jangwani hadi viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Taasisi ya Elimu
Tanzania iliratibu sherehe hii hadi 2006. Kuanzia mwaka 2007 sherehe hii
imekuwa ikiendeshwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA).
Tofauti na sherehe ya siku ya pai,
CHAHITA hakiratibu sherehe ya siku ya kadirio la pai. Sherehe hiyo imeachwa
kuwa huria. Shule na Taasisi zenye mapenzi na hisabati zinaweza kufanya sherehe
hiyo kwa mikakati ambayo itasaidia kuhamasisha wanafunzi kupenda somo la
Hisabati. Pengine kukosekana nguvu ya kitaifa ya CHAHITA ndiyo chanzo cha watu
wengi kutoijua siku hiyo lakini hata juhudi za binafsi husaidia.
Miaka michache iliyopita, mwalimu Eva Kwalazi Kipimo
wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana, aliwahi
kufanya sherehe hiyo katika Shule ya Uhuru Wasichana wakati alipokuwa anafundisha
hapo. Sasa ni mstaafu. Yeye aliita SIKU YA HISABATI na shule iliwaalika wazazi
kuona matukio mbalimbali ya Hisabati pamoja na zana za kufundishia/kujifunzia
somo hilo .
Baadhi yenu mtajiuliza kwa nini tunasema
kadirio la pai. Kwani thamani halisi ya pai ipi? Ili uielewe hiyo inakubidi
ujue pai ni nini, Pai si 22 juu ya 7 au
3.14 kama ulivyozoea kuamini. Haayo ni
makadirio tu na yanatosheleza kwa matumizi ya kawaida. Thamani kamili kwa
tarakimu bado haijapatikana. Wataalam wanaendelea kuitafuta
japoluwa imeshatafutwa kwa mamjilioni ya
nafasi za desimali. Wanachotafuta ni kujua ni lini tarakimu zitaanza kujirudia
ili wachunguze mtindo wa mtiririko na hatimaye kuunda kanuni.
Kimsingi tunajua kuwa pai ni mzingo wa
duara (mduara) gawanya kwa kipenyo chake. Unapogawanya unapata hisa kwa decimal.
Si rahisi kuipata kwa sehemu. Unaweza kujaribu mwenyewe kwa kupima vitu vyenye
umbo la duara. Pima mzingo kwa kuzungushia uzi
na hatimaye upime urefu wa uzi huo kwenye rula au metakamba.
Pima urefu wa
kipenyo (kumbuka mstari wa kipenyo hupita katikati) kisha gawanya mzingo
kwa kipenyo. Kadiria jibu lako kwa nafasi mbili za desimali. Fanya hivi kwa
vitu kama vinne kaisha tafuta wastani. Kama
umefanya kwa makini utapata jibu linalokaribia 3.14. Hilo ndilo kadirio lako la pai kwa kuwa
umelitafuta mwenyewe na una haki ya kujivunia, au sio?
Hebu sasa tuchunguze kadirio la 22 juu ya
7. Kwa nafasi tano za desimali, ukigawanya unapata 3.14286 wakati thamani
halisi kwa nafasi hizo za desimali ni 3.14159. Unaona jinsi namba hizo
zinavyotofautiana katika nafasi ya tatu ya desimali? Kwa hiyo 22 juu ya 7 ni
kadirio la pai. Nadhani tumekwenda pamoja mpaka hapo.
Sasa tuangalie utafanya nini siku hiyo
mwakani. Kama ni mwalimu utawakusanya
wanafunzi na kuwapa fursa ya kuimba nyimbo za Hisabati. Unaweza kuandaa maonesho
, kongamano au mdahalo wenye uhusiano
nna hisabati. Ikiwa wewe ni mkuu wa shule au chuo unaweza kualika mtaalamu wa
Hisabati karibbu na wewe kuwahamasisha wanafunzi kupenda Hisabati. Ukiwa ni
mdau wa kawaida changia mawazo yako kwa njia ya redio, televisheni na magazeti
. Tutafurahia mchango wako.
Ni
muhimukuzingatia hili maana wanafunzi wanahitaji kuhamasishwa . Sote tumeshuhudia jinsi wanafunzi
wanavyofeli katika somo la Hisabati kwenye mitihani ya Kitaifa. Fursa kama hii
itumikekuinuan kiwango cha ufanisi kwa somo hilo.
Mwaka huu magazeti mbalimbali yaliandka
makala kuhusu siku ya Pai ioiyofanyika Mnazi Mmoja, Pia TBC1 plimwalika mtaalam
wa pai kwenye kipindi cha Jambo asubuhj ya siku hiyo. Televisheni ya Channel
Ten nayo ilirusha habari za kadirio hilo
wakati wa mchana siku hiyo. Magazeti nayo yalilijizatiti kwa kuchapisha makala
ya sikuya pai Tanzania.
Mwalimu Albinus Balomi wa shule ya Sekondari
Kijitonyama amekuwa miongoni mwa watu wa
kwanza kutoa mrejesho. Yeye alibahatika kuona hicho kipindi cha TBC1 wakati
alipokuwa anajiandaa kwenda shuleni. “Nilifurahia sana maelezo yaliyotolewa na mtaalamu. Alinifundisha mengi kuhusu pai
kwa muda mfupi. Mimi ni mwalimu wa Historia na Jografia. Nilijiambia kwamba
Hisabati inafundishika kutokana na jinsi mtaalamu huyo alivyowasilisha mada
yake japo kwa muda mfupi tu. Wangemwongezea muda,” alidai mwalimu Albinus.
“Nilipokuwa njiani,” aliendelea kueleza,
“nilinunua magazeti. Nilikuta makala
nzuri za Siku ya Kadirio la pai. Niliitumia kuwaelezea walimu wa Hisabati ambao
kusema kweli hawakuwa wanaijua siku hiyo. Walihamasika sana”.
Kuna
baadhi ya shule zimeonyesha kuijua hiyo siku ya kadirio la pai. Kwa mfano Shule
ya Sekondari ya Bright Angles iliyoko
Mkuranga mkoa wa Pwani, iliahirisha sherehe ya siku hiyo hadi Jumamosi tarehe
27 Julai, ili iwashirikishe wazazi na wadau wengine. Shule imonyesha jitihada
za kuhamasisha wanafunzi kupenda somo la Hisabati. Shule
imeamua
kuwazawadia wanafuzi wote waliopata A katika mtihani wa wa Taifa wa mwaka huu kwenye somo la
Hisabati. Pia imemwalika mtaalamu mmoja wa Hisabati kuwahamasisha wanafunzi.
Kumbuka
kuwa pai ina matumizi mengi katika maisha yetu. Hata kama hukuwahi kulipenda
somo unaweza kutenga muda kidogo kuifurahia siku.
end
No comments:
Post a Comment